• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yatenga ardhi kwa ajili ya mradi wa mji usio na uchafuzi wa mazingira

    (GMT+08:00) 2018-12-07 09:25:18

    Serikali ya Rwanda imetenga hekta 620 za ardhi kwenye viunga vya mji wa Kigali, kwa ajili ya mradi wa majaribio wa kwanza wa mji usio na uchafuzi wa mazingira.

    Waziri wa mazingira wa Rwanda Bw. Vincent Biruta amesema mradi huo upo kwenye kilima cha Kinyinya, na unatarajiwa kuleta mtazamo mpya wa kuendeleza miji isiyo na uchafuzi, na itahusu kuweka kanuni mpya za maendeleo endelevu, sera mpya za vigezo vya majengo yasiyosababisha uchafuzi na usafiri wa kutumia umeme.

    Ujenzi wa nyumba 140 zisizosababisha uchafuzi utakuwa ni hatua ya kwanza ya mradi huo, na katika hatua ya pili nyumba za gharama nafuu zitajengwa kwenye eneo la hekta 250. Waziri huyo amesema hatua ya mwisho itahusisha ujenzi wa majengo ya ofisi na biashara, na inatarajiwa kuvutia biashara za kivumbuzi zisizosababisha uchafuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako