• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yafikiria sera dhidi ya biashara ya watoto

    (GMT+08:00) 2018-12-07 09:58:58

    Serikali ya Sudan Kusini imetangaza mpango wake wa kutekeleza sera ya uhamiaji ili kupambana na biashara haramu ya watoto.

    Naibu msemaji wa idara ya polisi ya taifa ya Sudan Kusini Bw. James Dak, amesema serikali inajadiliana na wanaharakati wa haki za binadamu ili kupata njia ya kutunga sera.

    Kwenye mazungumzo kuhusu ukatili wa kijinsia, Bw. Dak amesema serikali inalazimika kutunga sera ili kusaidia kuzielekeza idara za utekelezaji wa sheria kutatua masuala ya kuwateka watoto na biashara ya wasichana ambayo imeongezeka kwenye maeneo ya mipakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako