• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la serikali la Libya laonya dhidi ya mabadiliko ya mapema ya katiba ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2018-12-07 16:21:22

    Baraza la Juu la serikali ya Libya limeonya dhidi ya kufanya marekebisho ya katiba mapema, likidai kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha changamoto za kikatiba.

    Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imesema muswada wa marekebisho ya katiba bado unajadiliwa. Kauli hiyo imekuja baada ya mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya nchini humo Bw. Imad Al-Sayah kutangaza mapema jana kuwa kura ya maoni kuhusu katiba ya kudumu ya nchi hiyo itapigwa kabla ya mwisho wa mwezi Februari mwaka ujao. Mwezi Julai mwaka huu, Bunge la Katiba lilipitisha muswada wa marekebisho ya katiba ya nchi hiyo.

    Tangu kuanguka kwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi mwaka 2011, nchi hiyo imekumbwa na msukosuko katika harakati za kufanya mpito wa kidemokrasia kutokana na utengano, ukosefu wa usalama na vurugu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako