• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono kutumia fedha za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kusaidia operesheni za kulinda amani za Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-07 16:32:58

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu jana amesema,, China inaunga mkono kutumia fedha za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kwa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Afrika.

    Balozi Ma amesema, baadhi ya nchi na mashirika ya kikanda zinakosa uwezo wa kulinda amani na usimamizi kutokana na upungufu wa fedha, hivyo kuwa ngumu kutimiza amani ya muda mrefu na maendeleo. Ikiwa nchi kubwa ya pili inayotoa fedha za kulinda amani kwa Umoja wa Mataifa, China inaunga mkono fedha hizo zitumike katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Afrika, pia inalitaka Baraza la Usalama lifikie maoni ya pamoja mapema iwezekanavyo kuhusu suala hilo. Amesema China itaendelea kuuunga mkono Umoja wa Mataifa ufanye ushirikiano na Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kikanda kwa kupitia utoaji wa fedha na mfuko wa amani na maendeleo wa China na Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako