• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-12-07 18:46:39

    Rais Xi Jinping wa China hapa Beijing amekutana na waziri wa mambo ya nje ya Korea Kaskazini Bw. Ri Yong Ho.

    Rais Xi amesema, mwaka huu kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amefanya ziara tatu nchini China, na wamebadilishana maoni juu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya pande mbili, kuhimiza maendeleo ya amani na utulivu wa kikanda, huku akifurahia kuona makubaliano mbalimbali muhimu yaliyofikiwa na pande mbalimbali yakitekelezwa kihalisi.

    Bw. Li amesema, Korea Kaskazini inapenda kufanya juhudi pamoja na China kufanikisha maadhimisho ya miaka 70 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi mwakani ili kuimarisha urafiki wa kijadi, na ushirikiano wa pande mbili. Amesema Korea Kaskazini itaendelea kufanya juhudi kutimiza peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia huku ikipenda kudumisha mawasiliano na China kuhusu amani na utulivu wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako