• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutumia milioni 500 kujenga masoko ya mifugo

    (GMT+08:00) 2018-12-07 19:14:11

    Serikali ya Kenya itatumia kitita cha Sh500 milioni kujenga masoko ya mifugo kote nchini humo kuanzia mwaka ujao. Masoko hayo yatalenga maeneo ambayo kwa kawaida hayajulikani kwa riziki ya biashara za mifugo ili kuibua mtazamo wa kuekeza katika sekta hiyo miongoni mwa wenyeji.

    Masoko hayo yatajengwa katika maeneo bunge 35 kwa ushirikiano wa wafadhili, serikali za kaunti na serikali kuu.

    Hayo yalisemwa na afisa wa ustawishaji viwanda vya mashinani katika Wizara ya Ugatuzi Bw John Kamuto katika warsha ya wakulima iliyofanyika katika Shamba la Utafiti wa Kilimo la Jomo Kenyatta-Mareira lililopo katika Kaunti ya Murang'a.

    Bw Kamuto aliarifu wakulima hao kwamba masoko hayo yatakuwa yakizingatia biashara ya mifugo pekee.

    Kwa upande wake afisa wa ustawishaji wa mifugo katika Kaunti ya Murang'a Bw James Thuo Wainaina amesema kuwa mradi huo utashirikisha Kaunti zilizoko katika maeneo ya Nyanza, Mashariki na Kati.

    Bw Wainaina alisema kuwa sekta ya mifugo imeorodheshwa kama kiungo muhimu cha kuafikia mbinu za kuinua wakulima katika ruwaza ya 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako