• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Sudan Kusini wawasihi wananachi kusameheana baada ya vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe

    (GMT+08:00) 2018-12-08 18:15:26

    Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na naibu wake Wani Igga wapo kwenye kampeni ya pamoja wakitaka kuwaunganisha na kuwapatanisha watu wa Sudan Kusini waliosambaratika kutokana na mgogoro wa miaka mitano.

    Kwenye ujumbe wao uliorushwa kwenye redio za nchi hiyo, viongozi hao wamewasihi watu wa Sudan Kusini kusameheana ili kuweka njia ya mapatano katika taifa zima. Kwenye kampeni hiyo inayoongozwa na makundi ya kidini, yanatumika mabango na rikodi ili kueneza ujumbe wa amani nchi nzima.

    Wakati huohuo Mkurugenzi wa kitengo cha haki za binadamu cha Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, Eugene Nindorera ametoa wito wa kupanuliwa kwa nafasi ya kiraia ili kuendeleza utekelezaji wa makubaliano ya amani. Amesisitiza kuwa ushiriki mzuri wa kiraia, ikiwemo kukuza haki za binadamu, bado ni changamoto inayohitaji kutambuliwa na kutatuliwa kwenye kipindi hiki muhimu katika historia ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako