• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Mashariki yaahidi kuunganisha kodi ili kuendeleza soko la pamoja

    (GMT+08:00) 2018-12-08 18:16:18

    Mamlaka za mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki jana ziliahidi kuunganisha kodi zao za ndani ili kukuza soko la pamoja.

    Kwa mujibu wa tamko la pamoja lililotolewa mjini Nairobi baada ya kufungwa kwa mkutano wa 45 wa makamishna wakuu wa mamlaka za mapato za Afrika Mashariki na kamati ya pamoja ya uratibu wa kikanda, Mamlaka za mapato zimesema kuwa ili kurahisisha kwa ufanisi biashara na kuboresha maafikiano wamekubaliana kukuza mfumo wa pamoja wa usimamizi wa forodha utakaochukua nafasi ya mfumo wa sasa wa kila nchi kujitegemea.

    Wakuu wa mamlaka za mapato za kanda pia wametaka kuboreshwa zaidi kwa uwezo wa kukabili ukadiriaji wa chini, kwa kutekeleza haraka mfumo wa ukadiriaji wa fordha wa kielektroniki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao unawezesha kuweka alama ya thamani ya mizigo yenye bidhaa mbalimbali kutokana na data za makadirio yaliyopatikana kwenye mifumo ya taifa ya forodha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako