• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana kuhimiza mchakato wa siasa wa Syria

    (GMT+08:00) 2018-12-08 18:17:40

    Mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia suala la Syria Bw. Xie Xiaoyan jana alipohojiwa na vyombo vya habari huko Geneva alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana kuhimiza mchakato wa siasa wa Syria kupata maendeleo halisi.

    Bw. Xie Xiaoyan amesema, China siku zote inashikilia kutatua suala la Syria kwa njia ya kisiasa, kuunga mkono Umoja wa Mataifa kutekeleza jukumu lake muhimu la usuluhishi, na kuunga mkono juhudi za mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika suala hilo.

    Bw. Xie pia amesema, kwa sasa hali ya kibinadamu nchini Syria imeboreshwa, baadhi ya wakimbizi wameanza kurudi nyumbani, na pande mbalimbali zinajadili namna ya kusukuma mbele kazi ya ukarabati. Ingawa ugaidi upo na kutishia kanda hiyo na jumuiya ya kimataifa, lakini mapambano dhidi ya ugaidi yamepata mafanikio makubwa. Kutokana na hali hiyo, pande mbalimbali zinapaswa kutumia fursa hii, na kushirikiana kuhimiza suala hilo litatuliwe kwa njia ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako