• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yasema mazungumzo kuhusu Kordofan Kusini na Blue Nile kuanza Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2018-12-09 19:06:35

    Serikali ya Sudan imesema raundi mpya ya mazungumzo kuhusu maeneo ya Kordofan Kusini na Blue Nile, inatarajiwa kuanza jumapili mjini Addis Ababa.

    Msaidizi wa Rais wa Sudan Kusini Bw. Faisal Hassan Ibrahim amesema ujumbe wa serikali utaondoka jumamosi kwenda Addis Ababa, na uko tayari kufanikisha amani ya maeneo Kordofan Kusini na Blue Nile.

    Bw. Ibrahim amelitaka kundi la SPLM Kaskazini kuchagua amani ili kukomesha mateso yanayowakabili watu kwenye maeneo hayo mawili, kabla ya kuingia kwenye hatua ya kuanza kuandaa katiba na uchaguzi wa mwaka 2020.

    Mpaka sasa raundi 10 za mazungumzo ya amani kati ya serikali na kundi la upinzani la SPLM tawi la Kaskazini mjini Addis Ababa, kuhusu maeneo ya Kordofan Kusini na Blue Nile, yamefanyika chini usimamizi wa Umoja wa Afrika. Lakini mazungumzo hayo hayajapata mafanikio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako