• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wazindua miradi ya maendeleo nchini Ethiopia iliyojengwa na China

    (GMT+08:00) 2018-12-09 19:06:58

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw Abiy Ahmed, Rais wa Djibouti Ismal Gulleh na Rais wa Sudan Omar al-Bashir wamezindua eneo la viwanda la Jimma lililojengwa na China, lililopo mji wa Jimma kilometa 350 magharibi mwa mji wa Addis Ababa.

    Viongozi hao pia wameshuhudia kuwekwa kwa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa barabara unaojengwa kwa kandarasi ya China, wakati Ethiopia ikiwa na lengo la kuunganisha miji yake ya kimkakati kwenye eneo lake la magharibi ya Jimma, Agario na Dedesa.

    Eneo la viwanda la Jimma linajengwa na kampuni ya ujenzi ya China (CCCC) na linatarajiwa kuwa na viwanda vyepesi, hasa vya usindikaji wa vyakula na nguo.

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amesema eneo la viwanda la Jimma litasaidia kuifanya sehemu ya magharibi mwa Ethiopia kuwa kituo cha kiviwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako