• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Afrika lafunguliwa mjini Sharm el Sheikh kukiwa na matarajio makubwa

    (GMT+08:00) 2018-12-09 19:07:21

    Mkutano wa mwaka 2018 wa Baraza la Afrika umefunguliwa jana mjini Sharm El Sheikh nchini Misri ukihudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali wanachama wa soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika COMESA.

    Mkutano huo umeandaliwa kati ya serikali ya Misri na COMESA, na unatarajiwa kufanyika kwa siku mbili, ukijadili masuala yanayohusu miundo mbinu, ujasiriamali, uwekezaji na mambo yanayohusu wanawake barani Afrika.

    Katika siku ya kwanza, mkutano huo ulikuwa na mjadala kuhusu "siku ya ujasiriamali ya vijana" ukiangalia mambo ya kuimarisha ushirikiano wa biashara ya kuvuka mipaka, na kufungua masoko mapya kwa nchi za COMESA.

    Mjadala mwingine ulihusu kuwawezesha wanawake wa Afrika, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa usawa wa kijinsia katika kufanikisha maendeleo ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako