• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya magari ya Mwendokasi: Hamilton apewa tuzo ya ubingwa wa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-12-10 08:31:43

    Dereva wa mashindano ya magari ya mwendokasi mwingereza Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes amekabidhiwa rasmi tuzo ya ubingwa wa mbio za mwaka huu kwenye hafla iliyofanyika usiku wa jumamosi mjini St. Petersburg huko Urusi.

    Kwa msimu huu, Hamilton amejikusanyia alama 408 za ushindi, akifuatiwa na mjerumani Sebastian Vettel kutoka timu ya Ferrari aliyepata alama 320, na nafasi ya tatu ikichukuliwa na dereva mwingine wa Ferrari aliyepata Kimi Rikonnen wa Finland aliyepata alama 251.

    Huu ni ubingwa wa tano kwa Hamilton tangu aanze kushiriki mbio za magari, akifikia rekodi ya dereva wa zamani Juan Manuel Fangio kutoka Argentina, na rekodi ya ubingwa mara nyingi ikiwa bado inashikiliwa na Michael Schumacher aliyeshinda ubingwa mara saba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako