• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Palestina asisitiza haja ya kutelekeza maamuzi ya kuzipinga Israel na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-12-10 08:41:20

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesisitiza umuhimu wa kutekeleza maamuzi ya kuipinga Israel, Marekani na kundi la Hamas. Akiongea mjini Ramallah kwenye mkutano wa baraza la washauri la kundi la Fatah, Bw Abbas amesema kazi za kisiasa na kidiplomasia za Palestina, zinatakiwa kuzuia ukaliaji wa Israel dhidi ya watu na ardhi ya Palestina. Amesema ni lazima kutekeleza maamuzi ya baraza kuu la chama cha ukombozi wa Palestina PLO, kuhusu uhusiano na Israel, Marekani na Hamas.

    Wito wa Bw. Abbas umetolewa wakati wa-israel sita walijeruhiwa kwenye tukio la ufyatuaji risasi lililotokea katika eneo linalokaliwa la ukingo wa magharibi. Jeshi la Israel limesema risasi zilifyatuliwa na mtu aliyekuwa kwenye gari inayotembea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako