• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yazindua mfuko wa bima wa kuwahimiza wamisri kuwekeza barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-10 08:41:58

    Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri ametangaza kuzinduliwa kwa mfuko wa kukabiliana na hatari ili kuwahimiza wajasiriamali wa Misri kuwekeza barani Afrika.

    Akiongea kwenye sherehe ya ufungaji wa mkutano wa baraza la Afrika kwa mwaka huu uliofanyika mjini Sharm el-Sheikh, Rais al-Sisi ametangaza kuzinduliwa kwa mfuko wa uwekezaji kwenye miundo mbinu ya Tehama, kwa kutumia teknolojia za kisasa, ili kujenga uchumi wa kisasa.

    Zaidi wa wajasiriamali 3,000 wa Afrika walihudhuria mkutano huo, wakijadili masuala ya miundo mbinu, ujasiriamali, uwekezaji na mambo yanayohusu wanawake barani Afrika.

    Mapema jana Rais al-Sisi alisema Misri itaongeza uwekezaji wake barani Afrika, ambako kwa mwaka huu umeongezeka kwa dola bilioni 1.2 na kufikia dola bilioni 10.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako