• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yasaini mpango unaoungwa mkono na UN wa kupambana na ufisadi

    (GMT+08:00) 2018-12-10 08:45:34

    Somalia imejiunga na dunia kwenye maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya kupambana na ufisadi, kwa kusaini mpango unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa unaolenga kutokomeza tatizo hilo nchini humo.

    Wizara ya sheria ya Somalia na Shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP walisaini Mpango wa Kuanzisha Mradi wa PIP unaolenga kuimarisha taasisi za serikali kwenye mapambano dhidi ya ufisadi.

    Waziri wa sheria wa Somalia Bw. Hassan Hussein Haji amesema kupitia taarifa iliyotolewa na Tume ya Umoja wa mataifa nchini Somalia UNSOM, kuwa Somalia itachukua hatua za mfululizo kuimarisha mapambano dhidi ya ufisadi na kuongeza uwazi wa kazi ili kuzijenga taasisi za serikali ziwe za kuaminika.

    Imefahamika kuwa mpango huo wa PIP utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita, na baadaye UNDP itaanzisha programu ya kipindi kirefu ya kuiunga mkono serikali ya Somalia katika kupambana na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako