• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yatakiwa kuunga mkono mpango wa amani wa Darfur

    (GMT+08:00) 2018-12-10 09:13:00

    Tume ya kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya Doha kuhusu amani ya Darfur imeitaka jumuiya ya kimataifa iunge mkono mpango wa amani wa Darfur na miradi ya maendeleo kwenye kanda hiyo.

    Kwenye mkutano wa 14 wa tume hiyo uliofanyika huko Khartoum, mwenyekiti wa tume hiyo ambaye pia ni mjumbe maalumu wa waziri wa mambo ya nje wa Qatar kwenye kupambana na ugaidi na kusuluhisha migogoro, Bw. Mutlaq bin Majed al-Qahtani, amesema Darfur inashuhudia utulivu, lakini kukosekana kwa usalama bado ni changamoto kwa utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Darfur, hivyo kazi muhimu kwa sasa ni kunyang'anya silaha kutoka kwa wapiganaji na kuwarudisha kwenye jamii.

    Bw. al-Qahtani ameitaka jumuiya ya kimataifa itoe mchango zaidi ili kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano kuhusu amani ya Darfur, na kuanzishwa kwa miradi ya maendeleo kwenye kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako