• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lalaani ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-12-10 09:20:37

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake vilivyotokea hivi karibuni mjini Bentiu, kaskazini mwa Sudan Kusini.

    Baraza hilo limetoa taarifa likiwafuatilia wahanga hao, wakiwemo wanawake na wasichana zaidi ya 150 ambao walishambuliwa na watu wenye silaha kwenye eneo linalodhibitiwa na serikali mjini Rubkona.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini ilaani vitendo hivyo, na kuhakikisha inafanya uchunguzi na kuwajibisha wahusika. Baraza limesisitiza kuwa ni lazima kuwawajibisha watu waliokiuka sheria na haki za binadamu, na serikali ya Sudan Kusini ina wajibu mkuu wa kuwalinda wananchi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako