• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia yakataa ombi la Uturuki kuhusu kuwakabidhi watuhumiwa wawili wa kesi ya Jamal Khashoggi

    (GMT+08:00) 2018-12-10 17:00:19

    Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Bw. Adel al-Jubeir amekataa ombi la Uturuki kuhusu kuwakabidhi watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi kwa Uturuki.

    Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Riyadh, Bw. Jubeir amesema Saudi Arabia haitakabidhi raia wake kwa nchi za nje. Kauli hiyo imetokana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kutaka Saudi Arabia kuwakabidhi watuhumiwa hao ili kesi hiyo isikilizwe na kutolewa hukumu nchini Uturuki.

    Jumatano wiki iliyopita, Mwendesha mashtaka mkuu wa Uturuki alitoa amri ya kuwakamata raia wawili wa Saudi Arabia, Ahmad al-Assiri aliyekuwa naibu mkuu wa idara kuu ya upelelezi ya Saudi Arabia na Saud al-Qahtani, aliyewahi kuwa mshauri wa mfalme wa Saudi Arabia kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Bw. Khashoggi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako