• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema ufunguaji mlango zaidi wa China ni muhimu kwa kuchochea ukuaji wa uchumi

    (GMT+08:00) 2018-12-10 17:07:19

    Mchumi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Maurice Obstfeld amesema, ufunguaji mlango zaidi wa China kwa biashara ya kimataifa na uwekezaji utasaidia kuboresha ukuaji wa uchumi na utulivu, wakati nchi hiyo ikibadilika kuelekea ngazi ya maendeleo ya ubora wa juu.

    Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Bw. Obstfeld amesema sera ya China ya mageuzi na ufunguaji mlango iliyoanza kutekelezwa mwishoni mwa miaka ya 1970 imekuwa na athari chanya kwa kiwango cha maisha cha China. Amesema nyingi ya athari hizo zimeweka kugusa nchi nyingine, hususan Aisa Mashariki na sehemu nyingine zinazoibuka kiuchumi.

    Kama sehemu ya kuadhimisha miaka 40 ya sera hiyo, China imetangaza hatua mfululizo halisi za ufunguaji zaidi kwa uwekezaji wa kigeni, ikiwemo kuongeza upatikanaji wa soko, kuboresha mazingira ya uwekezaji, na kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako