• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ebola yaenea zaidi kwenye maeneo ya mijini nchini DRC

    (GMT+08:00) 2018-12-10 18:30:11

    Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola umeendelea kuenea katika maeneo ya miji mikubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF) imesema, mji ulioathiriwa karibuni zaidi na ugonjwa huo ni Butembo ambao uko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Mratibu wa mradi wa madaktari hao John Johnson amesema, wana wasiwasi mkubwa na hali ilivyo kwenye eneo la Butembo, na inabidi juhudi ziongezwe katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo.

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema, kesi mpya 35 za Ebola ziliripotiwa nchini DRC mpaka kufikia jumanne wiki iliyopita, huku kesi mbili mpya zikiripotiwa mjini Butembo, nane mjini Katwa, na mbili mjini Kalunguta.

    Mpaka kufikia ijumaa wiki iliyopita, takwimu zilizotolewa na WHO zimeonyesha jumla ya kesi za Ebola nchini DRC imefikia 489, huku 441 kati ya hizo zikithibitishwa kuwa ni maambukizi ya Ebola na watu 232 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako