• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 15 wafariki na wengine 31 waokolewa baada ya jengo la ghorofa kubomoka Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-12-11 08:59:17

    Idara ya kukabiliana na matukio ya dharura ya Nigeria imethibitisha kuwa miili ya watu 15 imepatikana na watu wengine 31 wameokolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo la ghorofa saba lililobomoka mwezi uliopita mjini Port Harcourt, kusini mwa Nigeria.

    Mratibu wa Idara hiyo Bw. Ejike Martins amesema umaalumu wa ajali hiyo ni kuwa ghorofa moja ilianguka moja kwa moja juu ya ghorofa nyingine, ndiyo maana kifusi kinaweza tu kuondolewa hatua kwa hatua.

    Jengo hilo lililoko kwenye Eneo la Serikali mjini Port Harcourt lilianguka wiki tatu zilizopita wakati ujenzi unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako