• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yahimizwa kuinua ubora wa bidhaa ili kuongeza uuzaji wa bidhaa zake China

    (GMT+08:00) 2018-12-11 08:59:44

    Kenya imehimizwa kuinua ubora wa bidhaa zinazotengenezwa nchini humo ili kuongeza nguvu ya ushindani kwenye soko la China wakati uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo unaendelea kuboreka.

    Mtaalamu wa mahusiano kati ya China na Afrika Bw. Cavince Adhere amesema Kenya ina nafasi nzuri ya kupunguza urari mbaya wa biashara na China, kama itachukua hatua kuinua ubora wa bidhaa zake hadi kufikia vigezo vya kimataifa.

    Kenya ilishiriki kwenye maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China CIIE yaliyofanyika mwezi Oktoba mjini Shanghai. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliongoza ujumbe wa ngazi ya juu kuhuduria maonesho hayo, ambapo alisaini makubaliano mbalimbali ili kutandika njia kwa ajili ya kuuza bidhaa za kilimo cha maua nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako