• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF laihimiza Somalia iendelee na mageuzi

    (GMT+08:00) 2018-12-11 09:50:04

    Shirika la fedha la kimataifa IMF limeihimiza Somalia iendelee na mageuzi ili kusaidia kufufua uchumi na kutimiza malengo ya maendeleo.

    Ujumbe wa IMF ulioongozwa na Bw. Mohamad EIhage ambaye alifanya ziara nchini Kenya kuanzia tarehe 1 hadi 6 mwezi huu, ambapo alikutana na maofisa wa fedha wa Somalia, na kufanya ukaguzi wa kwanza chini ya Mpango wa kujisimamia SMP, na kusema IMF iko tayari kuunga mkono ajenda za mageuzi ya Somalia, na mahitaji ya kuendeleza uwezo kwa njia ya kutoa msaada wa kiufundi na kuimarisha mafunzo.

    Ujumbe huo umekaribisha ahadi za serikali ya Somalia kuhusu kuboresha mfumo wa fedha katika muda uliobaki mwaka huu na mwaka 2019, kwa njia za kupanua faida kutokana na hatua mpya za kodi na kudhibiti matumizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako