• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Tetteh kutoka Ghana ateuliwa kuwa mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa UN kwenye Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-11 09:51:24

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Antonio Guterres amemteua Bibi Hanna Tetteh kutoka Ghana kuwa mwakilishi wake maalumu kwenye Umoja wa Afrika (AU).

    Bibi Tetteh amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Bibi Sahle-Work Zewde na kuwa mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa mataifa kwenye ofisi za Umoja wa Afrika. Bibi Zewde ameachia nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Ethiopia.

    Ofisi ya habari ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa imesema, Bibi Tetteh ana uzoefu wa miongo kadhaa kwenye mambo ya kitaifa, kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na ujuzi wa kuhimiza makubaliano kati ya wadau tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako