• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mradi wa bomba la mafuta haueleweki (Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi Tz)

    (GMT+08:00) 2018-12-11 18:59:01

    Wakati Serikali ikiwa imeanza kulipa fidia kwa wananchi walio katika maeneo litakakopita bomba la mafuta kutoka Tanga mpaka Hoima nchini Uganda, uhakika wa kukamilika mwaka 2020 upo shakani. Hilo limebainishwa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni alipokutana na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani kujadili mustakabali wa mradi huo. Alifafanua kuwa ilitarajiwa uamuzi wa uwekezaji kufanyika mwaka jana ili ujenzi wa bomba hilo ukamilike mwaka 2020, lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.

    Irine alisema kinachosumbua ni makubaliano ya usimamizi na mgawanyo wa mapato baina ya wadau wakuu ambao ni Serikali za Uganda, Tanzania na kampuni zinazoshirikiana kutoa mtaji ambazo ni Total Oil ya Ufaransa, China National Offshore Oil Corporation na Tullow Oil ya Uingereza. Wakati Irene akiwa na wasiwasi huo, Dk Kalemani alisema Tanzania imeshakamilisha tathmini ya mazingira, jiolojia, fiziolojia na uthamini wa mali za wananchi waliopo eneo linakopita bomba hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako