• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wamachinga wafurahia vitambulisho (Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi Tz)

    (GMT+08:00) 2018-12-11 18:59:23

    Wamachinga na wajasiriamali nchini Tanzania wameahidi kumuunga mkono Rais John Pombe katika juhudi zake za kuhakikisha kuwa wafanyibiashara hawa wadogo wanapata vitambulisho vya biashara zao. Agizo la rais la utoaji vitambulisho lilijiri baada yake kutoa amri nyengine ya maafisa wa usalama kutowahangaisha wafanyibiashara wadogo wadogo. Viongozi wa wafanyibiashara hawa wanasema kuwa kuna changamoto nyingi sana zinazowakumba wamachinga, na endapo zitasikilizwa basi vitambulisho zaidi ya 25,000 vitatolewa haraka. Kitambulisho kimoja kinalipiwa shilingi 20,000 Tsh kwa lengo la kuwatambua wafanyibiashara hao. Kwa kipindi kirefu, rais magufuli amekuwa akiagiza mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Tanzania TRA na halmashauri, kutowatoza kodi wafanyibiashara wadogo amabo mitaji yao haizidi shilingi 4M Tsh. Hata hivyo, utekelezaji wa amri ya rais haujatiliwa maanani. Utaratibu wa kuwatambua wafanyibiashara wadogo ulipitishwa na bunge kwa sheria ya Fedha ya mwaka awa 2017. Sheria hii amabyo licha ya kuwatambua kulingana na sehemu wanazofanyia biashara, inawapa wajasiriamali na wafanyibiashara wadogo fursa ya kulipa kodi na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako