• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji mkuu wa Somalia una msongamano mkubwa zaidi wa watu barani Afrika kutokana na mapigano

    (GMT+08:00) 2018-12-11 19:04:52

    Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, umekuwa mji wenye msongamano mkubwa zaidi wa watu barani Afrika kwa kuwa familia zinakimbilia mjini humo kutafuta hifadhi, ulinzi na msaada.

    Ripoti iliyotolewa leo na Kituo cha Kusimamia Wakimbizi wa Ndani cha Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC) imesema, jambo hilo limetokana na mapigano na majanga ya asili kati ya mwaka jana na mwaka huu. Kituo hicho kimesema, ukame, ushindani wa kupata rasilimali na mazingira duni ya maisha vimechochea mapigano katika maeneo ya vijijini, na kuwalazimisha watu wakimbilie Mogadishu.

    Watu hao wanawasili Mogadishu bila makazi, chakula, wala njia yoyote ya kuhudumia familia zao, hivyo msaada zaidi unahitajika kuhakikisha kuwa watu hao wana mahali salama pa kuishi, wakipata huduma muhimu za msingi za kibinadamu ili kuweza kuishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako