• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda na Tanzania zakubaliana kuharakisha ujenzi wa reli ya kuvuka mpaka kati yao

    (GMT+08:00) 2018-12-12 09:01:42

    Mawaziri wa ujenzi wa Rwanda na Tanzania wamekubaliana nchi zao kuharakisha mchakato wa ujenzi mradi wa reli ya SGR kati ya Isaka na Kigali, reli inayotarajiwa kupunguza gharama za usafirishaji, kuhimiza mafungamano na kuboresha huduma za kijamii kwenye eneo la Afrika Mashariki.

    Waziri wa ujenzi wa Rwanda Bw. Claver Gatete na mwenzake wa Tanzania Bw. Isack Kamwelwe wamesema hayo baada ya kukutana mjini Kigali.

    Bw. Kamwelwe amesema kwa sasa wanatafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, na sasa wanaangalia nia ya benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) kama ina uwezo na hamasa ya kufadhili ujenzi wa mradi huo.

    Reli ya Isaka-Kigali itakayokuwa na urefu wa kilometa 400, inatarajiwa kuiunganisha Rwanda na Bandari ya Dar es salaam, na kugharimu dola za kimarekani bilioni 2.5. Tanzania inatarajiwa kugharamia dola bilioni 1.3 na Rwanda inatarajiwa kutoa zilizobaki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako