• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Sudan lapitisha mswada wa kujiunga na AIIB

    (GMT+08:00) 2018-12-12 09:07:54

    Bunge la Sudan limepitisha muswada wa kujiunga na Benki ya uwekezaji wa miundombinu ya Asia AIIB.

    Shirika la habari la Sudan SUNA limesema muswada huo umepitishwa kwenye kikao cha jana kutokana na ripoti iliyowasilishwa na kamati ya mambo ya kifedha na kiuchumi ya bunge kuhusu kujiunga na AIIB.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Abdel-Rasoul ameeleza kuwa idadi ya nchi wanachama rasmi wa benki ya AIIB kwa sasa imefikia 57, mbali na nchi nyingine 30 zilizotoa ombi la kujiunga na benki hiyo, na kwamba tangu ilipoanzishwa mwaka 2014, benki ya AIIB imetekeleza miradi 28 katika nchi 28, yenye thamani ya dola bilioni 5.5 za kimarekani.

    Wabunge wa Sudan wamesisitiza umuhimu kwa Sudan kujiunga na AIIB, na wameipongeza China kwa juhudi inazofanya katika kuhimiza uwekezaji nchini Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako