• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Ethiopia kuzindua eneo la viwanda lililojengwa na China

    (GMT+08:00) 2018-12-12 09:08:42

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed anatarajiwa kuzindua eneo la viwanda la Dire Dawa lililojengwa na China mashariki mwa nchi hiyo, kwenye hafla ya uzinduzi itakayofanyika Jumapili.

    Eneo hilo la viwanda la Dire Dawa lililojengwa na kampuni ya uhandisi wa ujenzi ya China CCECC kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 51, linatarajiwa kupokea wawekezaji wa sekta za nguo, ngozi na ujenzi. Eneo hilo pia linatarajiwa kutoa nafasi za ajira kwa waethiopia elfu 40.

    Naibu maneja wa Kundi la Maeneo ya Viwanda chini ya Ofisi ya kampuni ya CCECC nchini Ethiopia Bw. Zhu Lei, amesema CCECC imejenga na kuzindua maeneo ya viwanda vya Hawassa, Kombolocha na Adama, na hivi sasa imekamilisha asilimia 70 ya ujenzi wa eneo la viwanda la Bahir Dar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako