• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajasriamali wa Afrika waangazia majukwaa ya kidigitali kupanua biashara zao

    (GMT+08:00) 2018-12-12 09:46:42

    Mkutano wa kwanza wa biashara za kielektroniki barani Afrika unaofanyika kwa siku tano mjini Nairobi, Kenya, unaendeshwa kwa pamoja na Kenya, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya, ambapo mawaziri wa serikali, maofisa waandamizi wa kampuni, wavumbuzi, wachunguzi na wawekezaji wanajadili mkakati mpya wa kuhimiza maendeleo ya uchumi wa kidigitali barani humo.

    Wajasiriamali wa kizazi kipya barani Afrika wanapenda kutumia fursa zinazoletwa na majukwaa ya kidigitali kupanua shughuli zao barani humo. Kwenye mazungumzo kuhusu biashara na uchumi wa kidigitali, waanzilishi wa kampuni za mitaji barani Afrika wamesema, biashara ya mtandaoni itaimarisha uwezo wa kampuni za asili.

    Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Afrilabs ya Nigeria Bibi Anna Ekeledo amesema, matumizi ya majukwaa ya kidigitali yatazifanya kampuni za huko zipanue masoko na kuongeza vyanzo vya mapato.

    Kwenye mkutano huo Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wajasiriamali vijana barani Afrika watumie fursa zinazoletwa na mapinduzi ya kidigitali na kuhimiza biashara ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako