• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wadau wa sekta binafsi waomba marekebisho ya utungaji wa sera za fedha

    (GMT+08:00) 2018-12-12 18:31:29

    Wadau wa sekta binafsi nchini Tanzania wamekuwa na maoni tofauti baada ya hotuba ya Rais John Magufuli aliyezitaka mamlaka za usimamizi nchini kufanya kazi kwa weledi ili kuhamasisha uwekezaji.

    Katibu mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Godfrey Simbeye amesema licha ya kupunguza wingi na viwango vya kodi kama Rais alivyoagiza, ipo haja ya kurekebisha utungaji wa sera za fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) isiwe mtungaji na msimamizi kwa wakati mmoja.

    Naye mwenyekiti mstaafu wa Jukwaa la Wakurugenzi wa Sekta Binafsi (CEOrt), Ali Mufuruki alisema tatizo kubwa lililopo nchini ni udhaifu wa sekta binafsi.

    Makamu wa rais wa Chama cha Wasafirishaji (TAT), Omar Kiponza alisema hoja ya askari kuwapotezea muda wafanyabiashara wanaoenda nje ya nchi imetolewa wakati muafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako