• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jaribio la kumwangusha rais wa Somalia lashindikana

    (GMT+08:00) 2018-12-12 19:27:32

    Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na rais wa Somalia Abdullahi Mohamed Farmajo iliyowasilishwa na wabunge nchini humo imetangazwa kuwa ni batili baada ya baadhi ya wabunge walioripotiwa kusaini wamekanusha kuiunga mkono.

    Katibu mkuu wa bunge la Somalia Abdikarim Haji Buh amebainisha kuwa, jumla ya wabunge 14 kati ya wabunge 92 wamesema hawakusaini hoja hiyo ya kutokuwa na imani na rais huyo na kudai imewasilishwa bila idhini yao.

    Buh ameeleza kuwa, idadi ya wabunge waliobaki haikutosha kutimiza akidi kulingana na kifungu cha 92 ibara ya 2 ya katiba ya Somalia.

    Jana jumanne, Spika na naibu wake walisema hoja hiyo ya kutokuwa na imani na rais alioko madarakani kunaweza kusababisha mgogoro wa kisiasa usiohitajika nchini humo na kwamba hakuna mahakama ya kikatiba ya kusimamia uhalali huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako