• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yasema Afrika Kusini inajaribu kuchelewesha mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida

    (GMT+08:00) 2018-12-13 09:14:36

    Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda imesema Afrika Kusini inaendelea kujaribu kuchelewesha au kukwamisha mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya nchi mbili.

    Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Rwanda imesema kupitia taarifa yake kuwa, ina wasiwasi na "mwendelezo wa majaribio" yaliyofanywa na wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini kuchelewesha au kukwamisha mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya nchi mbili.

    Taarifa imesema wasiwasi huo ni pamoja na "shutuma zisizo na msingi" dhidi ya Rwanda zilizotolewa kupitia taarifa za wazi au vyombo vya habari, kutokana na "uvumi na upotoshaji uliofanywa na wapotoshaji wa Rwanda walioko nchini Canada na Afrika Kusini, na vyombo vya habari vyenye uhusiano nao".

    Uhusiano kati ya Rwanda na Afrika Kusini ulikwama baada ya Afrika kusini kuwafukuza wanadiplomasia watatu wa Rwanda mwaka 2014 kutokana na shambulizi lililofanywa dhidi ya nyumba ya jenerali mstaafu wa Rwanda mjini Johannesburg, na Rwanda ikalipiza kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia sita wa Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako