• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watenga dola milioni 10 kudhibiti homa ya Ebola Afrika ya kati

    (GMT+08:00) 2018-12-13 09:15:02

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Bw. Mark Lowcock ametangaza kutolewa kwa dola milioni 10 za kimarekani kwa ajili ya kusaidia kudhibiti homa ya Ebola kwenye eneo la Afrika ya kati.

    Taarifa iliyotolewa na Mfuko wa dharura wa usaidizi wa Umoja wa Mataifa, CERF imesema fedha hizo zilizotolewa na mfuko huo zitatumika kupunguza athari zinazoweza kutokea za mlipuko wa homa ya Ebola unaoendelea, endapo homa hiyo itaenea kwa nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Fedha hizo ni nyongeza ya dola milioni 4.5 za kimarekani zilizotolewa na CERF kwa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini DRC wakati mlipuko wa homa ya Ebola ulipoibuka mwanzoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako