• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua mradi wa kwanza wa nishati ya jua wa kwenye uwanja wa ndege katika eneo la Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-12-13 09:15:24

    Kenya imekuwa nchi ya kwanza katika eneo la Afrika mashariki kuweka mfumo wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua kwenye uwanja wa ndege, kwa lengo la kupunguza utoaji wa kaboni wa ndege kubwa wakati zinapopaa.

    Mfumo huo wenye uwezo wa kuzalisha kilowati 500 za umeme, uliozinduliwa jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi mjini Mombasa, utasaidia kupunguza utoaji wa tani 1,300 za gesi za kaboni.

    Mkurugenzi wa Baraza la Shirika la usafiri wa anga la kimataifa ICAO Bw. Olimuyiwa Aliu, amesema haya sio tu ni maendeleo ya kimageuzi kwa sekta ya usafiri wa anga ya Kenya na Afrika, bali pia ni mfano wa kusisimua wa jinsi mabadiliko hayo yanavyotimizwa.

    Imefahamika kuwa mfumo huo utatoa hewa iliyoshughulikiwa na umeme uliozalishwa kwa nishati ya jua kwa ajili ya ndege kwenye operesheni zake za ardhini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako