• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya sintofahamu kuhusiana na chaguzi huwa na madhara kwa uchumi wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-13 09:30:39

    Hali ya kutokuwa na utulivu ambayo huwa katika kilele cha pilika za uchaguzi kwenye baadhi ya nchi za Afrika, imetajwa kuathiri vibaya ongezeko la uchumi wa nchi za Afrika.

    Ripoti iliyotolewa na taasisi ya wahasibu wa England na Wales kwa kushirikiana na wakadiriaji wa Oxford, inasema hali hii huwa inaathiri pato la taifa kwa baadhi ya nchi, kwa kuwa ongezeko la uchumi lina uhusiano wenye utatanishi na chaguzi na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa.

    Hata hivyo ripoti hiyo imesema nchi nyingi za Afrika zina matarajio mazuri ya ongezeko la uchumi, mbali na hali hizo nchi za Afrika zina matarajio mazuri ya ongezeko la uchumi.

    Ripoti hiyo inasema nchi za Afrika Mashariki zinaendelea kuwa na ongezeko kubwa la mapato licha ya kuwa mwaka huu ongezeko la uchumi kwa eneo hilo, linatarajiwa kupungua kutoka asilimia 6.7 ya mwaka jana na kuwa asilimia 6.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako