• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya ndege ya Afrika kupata hasara ya dola milioni 300 mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-13 19:18:43

    Shirikisho la kimataifa la usafiri wa anga IATA limesema kuwa mashirika ya ndege ya Afrika yatapata hasara ya dola milioni 300 mwaka 2019.

    Lakini hata hivyo IATA imesema hasara hiyo ni ya chini ikilinganishwa na dola milioni 400 za mwaka 2018.

    Hasara inayotokana na kila abiria ni dola 3.51 na hivyo kuyafanya mashrika ya ndege ya Afrika kuwa yanayofanya vibaya ikilinganishwa na mengine duniani.

    Na kwa jumla kote duniani IATA inatarajia sekta ya usafiri wa anga kupata faida ya dola bilioni 35.5 mwaka ujao.

    Mwaka 2018 faida ya mashirika kote duniani ilikuwa dola bilioni 32.3, na ukuaji wa mwaka ujao unachangiwa na kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako