• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Uchumi wa Rwanda wakua kwa asilimia 7.7 robo ya tatu ya 2018

    (GMT+08:00) 2018-12-13 19:19:03

    Uchumi wa Rwanda ulikua kwa asilimia 7.7 katika robo ya tatu ya mwaka wa 2018, kutokana na utendaji mzuri wa sekta za huduma na viwanda.

    Taasisi ya Taifa ya Takwimu ya Rwanda (NISR) imesema ukuaji huo unaendanda na malengo ya ukuaji wa kila mwaka wa asilimia 7.2.

    Mkurugenzi Mkuu wa NISR Yusuf Murangwa, amesema sekta ya utoaji huduma imekua kwa asilimia 48 na kuwa mchangiaji mkuu wa uchumi ikifuatiwa na kilimo kinachochangia asilimia 28.

    Kati ya Julai na Septemba 2018, sekta ya huduma ilikua kwa asilimia 12, na kilimo kwa asilimia 5.

    Kulingana na ripoti ya taasisi hiyo, shughuli za viwanda ziliongezeka kwa asilimia 10 na ujenzi asilimia 17.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako