• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wakulima wa kahawa mbeya wateta kucheleweshwa malipo

  (GMT+08:00) 2018-12-13 19:19:22

  Wakulima wa kahawa katika mkoa wa Mbeya nchini Tanzania wameanza kupanda miche mipya bila kutumia mbolea kutokana na kukosa fedha baada ya vyama vya ushirika kushindwa kuwalipa.

  Wakulima hao wanasema licha ya kuwa walipeleka kahawa yo kwenye vyama vya ushirika lakini bado hawajapokea malipo yao hadi msimu wa kupanda.

  Sasa wanaiomba serikali kuingia kati ili wapate malipo yao na kuendelea na kilimo.

  Akijibu hoja hiyo ya kutolipwa wakulia wa kahawa, mweka hazina wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Mpakani Kalinga alisema hakuna fedha ya wakulima iliyopitia kwenye halmashauri baada ya bodi ya kahawa kuuzkahawa ya wakulima.

  Anasema bodi ya kahawa inapeleka fedha zote kwenye vyama vya ushirika ili zipelekwe kwa wakulima baada ya kukata makato yote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako