• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar: Zanzibar kuboresha sekta ya uvuvi baharini

    (GMT+08:00) 2018-12-13 19:20:59

    Waziri wa maliasili na mifugo wa Zanzibar Rashid Ali Juma amesema serikali inapanga kutumia bahari ipasavyo ili kuhakikisha inaimarisha uchumi wake.

    Pia amesema serikali inapanga kuboresha shirika la samaki la ZAFIKO kuwa la kisasa.

    Amesema ndani ya miezi minne ijayo, serikali itatoa meli mbili za uvuvi kwa shirika hilo kama sehemu ya oboreshaji wake.

    Meli hizo tayari zimeanza kujengwa na moja itakuwa kisiwani pemba na nyingine Ugunja.

    Zaidi ya watu 140,000 kisiwani humo wanategemea uvuvi kujikimu kiuchumi lakini pia wanakabiliwa na uosefu wa miundo msingi ya kufanya kazi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako