Serikali ya kaunti ya Mombasa nchini Kenya inatenga shilingi bilioni 1.6 za mradi wa kusafisha maji ya bahari kwa matumizi ya nyumbani.
Gavana wa kaunti hiyo Hassan Joho amesema mradi huo utakamilika mwaka 2021.
Mradi huo utatekelezwa na kampuni ya Hipania ya Almar Water Solutions.
Mitambo kwenye mradi huo itasafisha mita 100,000 za ujazo kila siku na kusambaza maji kwa zaidi ya watu milioni 1.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |