• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Ligi Kuu ya Australia yaongeza timu mbili

    (GMT+08:00) 2018-12-14 09:33:00

    Viongozi wa soka wa Australia jana walitangaza klabu mpya mbili, moja kutoka jijini Sydney na nyingine Melbourne zitakazoshiriki Ligi Kuu (A-League), ukiwa ni mpango wa kuanzisha upinzani mpya na fursa kwa wachezaji. Mpango wa kuongeza timu kwenye A-League hadi kufikia 12 ni wa miaka mingi na mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Australia, Chris Nikou alitangaza washindi wa zabuni hiyo kati ya waombaji sita kuwa ni kampuni za ubia kutoka Melbourne Magharibi na Sydney Kusini-Magharibi, huku waombaji kutoka Canberra wakipigwa chini. Mpango huo utatekelezwa ndani ya misimu miwili, Western Melbourne ikiingia msimu wa mwaka 2019/20 na Sydney mwaka mmoja baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako