• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Gregg Popovich awa miongoni mwa makocha watano walioshinda mechi nyingi za NBA

    (GMT+08:00) 2018-12-14 09:33:20

    Namalizia kwa kuangazia NBA. Kocha wa timu ya Kikapu ya San Antonio Spurs, Gregg Popovich ameingia kwenye rekodi za ligi ya kikapu nchini Marekani, baada ya kuwa kocha wa nne kati ya watano walioshinda mechi nyingi zaidi katika ligi hiyo. Gregg Popovich alikabidhiwa kijiti cha ukocha mkuu wa San Antonio Spurs mwaka 1996 akitokea Golden State Warriors ambayo alikuwa kocha msaidizi chini ya Don Nelson kuanzia mwaka mwaka 1994. Gregg Popovich ambaye sasa ameshinda mechi 1,211 pia yupo kwenye orodha ya makocha walioshinda mataji mengi katika ligi ya kikapu ya NBA akiwa ameweka kabatini mataji matano yote akiwa na timu ya San Antonio Spurs. Makocha wengine ni pamoja na Don Nelson ameshinda mechi 1335. Lenny Wilkens ameshinda mechi 1332. Jerry Sloan ameshinda mechi 1221 na Pat Riley ameshinda mechi 1210.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako