• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mambo matatu muhimu kuhusu uchumi wa China katika mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-14 18:13:56

    Ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China jana imefanya mkutano wa kupanga kazi ya uchumi ya China katika mwaka 2019. Kutokana na habari zilizodokezwa kwenye mkutano huo, mambo matatu muhimu yanastahili kufuatiliwa.

    Kwanza, ni kujiendeleza kwa hatua madhubuti.

    Mkutano huo umesema, kuimarisha hali ya ajira, mambo ya fedha, biashara ya nje, mitaji ya nje na uwekezaji, na matarajio, kudumisha uchumi uendelezwe vizuri na utulivu wa hali ya jumla ya jamii, kuimarisha mkakati na kujiendeleza kwa hatua madhubuti. Hayo yote yanaonyesha kuwa uongozi wa chama unafahamu mabadiliko ya sasa ya mazingira ya ndani na nje, pia una imani ya kukabiliana nayo. Hasa kutokana na kuongezeka kwa msukosuko wa biashara duniani na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika wa ongezeko la uchumi duniani, "kujiendeleza kwa hatua madhubuti" ni muhimu sana kwa China. Pia China yenye maendeleo tulivu itaendelea kuwa nguvu ya ongezeko la uchumi duniani.

    Pili, ni maendeleo yenye sifa bora

    Mkutano huo umesema, China imetimiza maendeleo yenye sifa bora, na wananchi wamepata manufaa zaidi. Mwaka kesho, "maendeleo yenye sifa bora", "kuinua hisia ya wananchi ya kupata manufaa, furaha na usalama" pia zitakuwa lengo la kujiendeleza kiuchumi la China. Kwa hiyo, China itaendelea kufanya mageuzi ya miundo ya uchumi, kuzidisha mageuzi yanayozingatia soko, kupanua kiwango cha kufungua mlango, kuharakisha ujenzi wa mfumo wa uchumi wa kisasa, kutilia mkazo kinga na utatuzi wa hatari kubwa, kuondoa umaskini kwa usahihi, mapambano dhidi ya uchafuzi, sekta ya uzalishaji, soko la ndani, ustawi wa vijiji, utaratibu wa kikanda, mageuzi ya mfumo wa uchumi, na maisha ya wananchi. Inatazamiwa kuwa, kupanua mahitaji ya ndani na kuimarisha uchumi halisi kutakuwa na umuhimu zaidi kwa ongezeko la uchumi la China mwaka kesho.

    Tatu, ni kushikilia kufanya kazi wenyewe

    Katika mwaka 2019, China itaendesha mkutano wa pili wa baraza la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", maonyesho ya pili ya CIIE. Katika suala la maendeleo, China siku zote inafanya kazi kwa kufuata hali yake yenyewe na mpango wake yenyewe, bila kujali mabadiliko ya hali ya nje, na haitafanya mabadiliko yoyote. Mkutano huo umesema, inapaswa kutumia fursa muhimu ya maendeleo, kuimarisha imani, na China kushikilia kufanya kazi zake yenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako