• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hakuna majadiliano mapya katika mpango wa Brexit: Viongozi wa EU waiambia Uingereza

    (GMT+08:00) 2018-12-14 19:02:40

    Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameweka wazi kwa waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May kuwa hakuna makubaliano mapya juu ya mkataba wa Brexit.

    Viongozi hao wapo mjini Brussels kwa mkutano wa siku mbili ambapo ajenda kuu ni kuhusu Brexit, bajeti mbalimbali za mwaka na uhamiaji.

    Rais wa baraza la mawaziri la Ulaya Donald Tusk akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jana amesema kuwa Umoja wa Ulaya unashikilia kwamba hakuna kitakachobadilishwa katika mpango huo na inasimamia mkataba huo.

    Mkutano huo unakuja siku chache baada ya May kuepuka kuangushwa katika kura ya kutokuwa na imani nae kutoka kwa wabunge wa chama chake cha Conservative, ambao wengi wao walikasirishwa na waziri mkuu huyo na mpango wake wa kutaka Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako