• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi ya simu kuwasaidia kuwainua wanawake kiuchumi

    (GMT+08:00) 2018-12-14 19:28:58

    Utafiti uliofanywa hivi majuzi umebaini kuwa matumizi mazuri ya simu za mkononi miongoni mwa wanawake si tu yatawasaidia kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia bali yametajwa kusaidia kaya masikini kuinua kipato.

    Utafiti mpya uliofanywa na Taasisi ya Repoa umebaini kuwa, asilimia 70 ya wanawake kwenye kaya masikini waliweza kutumia simu kwaajili ya shughuli za maendeleo.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo ulioitwa 'Umiliki na Matumizi ya Simu miongoni mwa Wanawake', Mkurugenzi wa Repoa,Dk Donald Mmari amesema kaya masikini zinaweza kusaidiwa kwa kumwezesha mwanamke kutumia teknolojia ya simu katika shughuli zake.

    Utafiti huo ambao ulihusisha wanawake 2,000 kutoka mikoa ya Arusha, Iringa,Mwanza, Tanga na Ruvuma ukizingatia kaya masikini ili kuona jinsi matumizi ya huduma za kibenki (Simu-bank) zinavyoweza kuchochea maendeleo.

    Utafiti pia unasema simu imeleta matokeo chanya kwa wanawake kuwasaidia kuzifikia fursa mbalimbali za maendeleo.

    Asilimia 70 ya wanawake hao walizitumia simu kwa ajili ya shughuli za kiuchumi ikiwamo kununua pembejeo, kuanzisha biashara pamoja na kufuatilia taarifa za masoko ya bidhaa.

    Hatahivyo, utafiti huo umebaini kuwa asilimia 30 ya wanawake kutoka kwenye kaya hizo walipoteza simu kutokana na sababu mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako