• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wapunguza kasi ya ufanisi katika bandari ya Dar es salaam

    (GMT+08:00) 2018-12-14 19:29:20

    Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko amesema wadau wake wa karibu wanawapunguzia kasi ya ufanisi katika bandari hiyo. Kauli hiyo inakuja muda mfupi tu baada ya Rais John Pombe Magufuli kuzitaja mamlaka kadhaa ambazo zinachangia kudumaza mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini humo kuzorotesha ukusanyaji mapato,.

    Kakoko amesema TPA inatekeleza maagizo ya Rais lakini akazitaka taasisi nyingine zinazohusika na shughuli bandarini kuboresha utendaji wao.

    Katika Bandari ya Dar es Salaam, alisema zipo taasisi 36 za umma na wizara saba jambo ambalo limekuwa likikawiza utoaji wa shehena kwenye bandari hiyo.

    Alisema endapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake kwa wakati, TPA haiwezi kuzuia mzigo kutoka bandarini kwa kuwa wafanyabiashara ni wadau muhimu wa uchumi wa Taifa.

    Alisema tayari hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwamo kuzifungia kampuni za uwakala wa forodha zinazochelewesha utoaji wa mizigo kwa makusudi.

    Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Fedha pamoja na TRA kushirikiana katika kuongeza wigo wa mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako