• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yaalika kampuni za kigeni kuwekeza kwenye sekta ya madini

    (GMT+08:00) 2018-12-14 19:29:58

    Serikali ya Zimbabwe imezialika kampuni za kigeni kuwekeza kwenye sekta ya madini nchini humo.Waziri wa madini wa Zimbabwe Winston Chitando amesema Zimbabwe ni nchi ambayo ina utajiri mkubwa wa madini na ingependa kushirikiana na kampuni za kigeni ambazo ziko tayari kuwekeza kwenye sekta hiyo.Kauli hiyo inakuja wakati ambapo Zimbabwe imekuwa ikijitahidi kurudisha imani ya wawekezaji ambayo ilikuwa imepotea baada ya wazungu kupokonywa mashamba yao na kukabidhiwa watu weusi chini ya utawala wa Robert Mugabe. Chitando amesema hivi karibuni wataruhusu kampuni mbili kuwekeza kwenye sekta ikiwa ni mwanzo tu wa mabadiliko ya kurudisha imani ya wawekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako